Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5[ImagesOnly]

Style6

Anne Kansiime kutoa burudani siku ya Jumamosi Golden Tulip

Mchekeshaji Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi.

‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.

Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.

‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.

Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.
Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band.


Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia.

‘Usiku wa leo ni maalumu kwa watanzania kufurahia utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.

Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.  

New Music: Deddy - Tujimwage


New Music: Usikilize mkwaju mpya wa Dudu Baya "NIOKOE"


Ni time yako kusikiliza single mpya ya Dudubaya, msanii mwingine wa longtime kwenye bongofleva ambae jina lake lipo kwenye list ya Wasanii wa bongofleva waliowahi kumiliki Top10 kwa hits kama ‘nakupenda tu’ na ‘mwanangu huna nidhamu’

BAADA YA KUPOROMOSHA BURUDANI YA NGUVU EID MOSI, LEO SKYLIGHT BAND KAMA KAWAIDA NDANI YA THAI VILLAGE NJOO USIKOSEE

Digna Mbepera (wa kwanza kushoto)akiimba kwa hisia kaliiiii ndani ya kiota cha maraha na burudani Thai Village Masaki,Kulia kwake ni Aneth Kushaba akimpa sapoti ya ukweli.Kila ijumaa Skylight Band wanakuwa Thai Village wakitoa burudani ya nguvu yenye kukonga roho yako kwa muziki mzuri na uliopangiliwa sawa sawa, Ijumaa ya leo kama kawaida njoo ufurahi na ukutane na marafiki wapya.

Mary Lucos mwadada mwenye sauti tamu na nyororo akiimba kwa raha zake kuwapa burudani mashabiki wake.

Aneth Kusha a.k.a AK47 au Le meneja her self akiimba kwa furaha kabisa ndani ya Thai Village kuwapa mashabiki wake burudani ya nguvu.

Sam Mapenzi akipiga vocal za ukweli kwa hisia kaliii

Hashimu Donode akiwarahatupisha mashabiki wake kwa vocal kaliiii na tamu

Mary Lucos akipiga zile vokali nzito zilizoshiba ndani ya Thai Village ijumaa iliyopita.

Digna Mbepera akiimba taratibuuuu kwa vitendo kuwapa burudani yakutosha mashabiki wake ndani ya Thai Village ijumaa iliyopita usikose Leo kwa Mtonyo mdogo tuuuu.

Skylight Band Divas Wakishirikiana kwa pamoja kutoa vocal tamuuuuuuu ndani ya kiota cha maraha Thai Village Ijumaa iliyopita,Wa kwanza kushoto ni Mary Luvcos, Digna Mbepera(katikati)na Wa kwanza kulia ni Aneth Kushaba.

Majembe ya kazi wakiwajibika jukwaaani ili kutoa burudani ya nguvu kwa Mashabiki wao ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita wa kwanza kushoto ni Joniko Flower akifuatiwa na Sony Masamba(katikati)na wa mwisho kutoka kulia ni Sam Mapenzi.

Muziki ni furaha,hapo pichani ni mpiga tumba nambari moja kwa sasa Tanzania Daudi Tumba akifurahia kazi yake kwa raha mnooooo, Hii ndio Skylight bwanaaaa.

Mpiga kinanda mahiri wa Skylight Band Amos Kinanda akizipga nota zake vizuriiii kabisaaaa kutoa ala tamu kwa mashabiki wake ndani ya Thai village.

Anaitwa Idrisaaa hapo akizicharanga Drums zake kwa Rahaaa ili kuwapa Burudani mashabiki wake.
Ebwana Ehh anaitwa Allen Kiso hapo akizipiga kisu nyuzi za gitaa lake la solo kwa furaha na umakini mkubwa ili kuwapa burudani mashabiki wake.

Poziii kwa Poziiii anaitwa Mozee Vinanda hapo akionyesha mikogo kwa rahaaa zake namna kinanda kinapigwa ili kuwapa muziki mzuri mashabiki wakeee.

Tophy mabass huyu ni mpiga Bass gitaaa wa Skylight Band akizicharanga nyuzi za gitaa lake kwa umakini na furaha teleee.

Hapo sasaaaa mashabiki wakicheza kwa rahaaaa zaoooooo
Sugua suguaaaa mguuu wa kushoto mbeleeeeee,mguu wa kulia nyumaaaaaaa hapo mashabiki wa Skylight band wakifurahia mastyle makaliiii toka kwa wanamuziki wa Bendi

Kwa Rahaaaaa zao wakiserebuka njoo nawewe Ijumaa ya leo ufurahie muziki mzuri.

Le Meneja Her Self Aneth Kushaba Akifurahia Ukodak wa nguvuuuuuu toka kwa lenzi zetu

Le Meneja Her Self Akifurahia Muziki mzuriiiii toka kwa vijana wake ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera akiwa back stage akifurahia ukodak wa kamera zetuuu.

Digna Mbepera wa kwanza kushoto akiwa na Mary lucos Wakipata ukodak.

Hapooooooooooo Sasaaaaa Mashabiki wa Skylight Band wakifurahi kwa rahaaaa zao
Shabiki si akadataaaa kwa muziki mzuri wa Skylight Band akaanza kucheza kwa madahaaa na Sam Mpenzi.

Shabiki si akadata na Muziki mzuri wa Skylight Band, akasema msinitanieeeeee akapanda jukwaaani akaanza kucheza kwa rahaaaaa kabisa na sam Mapenzi

Happyyyyy Hapyyyyy Hapyyyyyyyyyyy mashabiki wa Skylight Band wakiimbishwa na Aneth Kushaba kwa rahaaaaa zaooo
Donode naye mzuka ukapandaaaaa akaenda kuimba na mashabiki.
28
Nyomi lakutoshaaaaa.....!

Le meneja Her Self Aneth Kushaba akiwajibikaaa vyakutoshaaa kwenye jukwaaa

Weweeeeeeee weweeeeee hapana chezea Aneth Kushaba wewe hapo akionyesha umahiri wa kudansiiii.

Hiii ndio Skylight Band bwanaaaa wakali wa majukwaaa ya dansi tanzania Hapo ni Aneth Kushaba akiwajibika sawa sawiiiiiiii

Daudi Tumba alimkunaaaaa vilivyo Meneja Aneth Kushabaaaaaa mpaka akatunzwaaa.

Sisi hatukosi Skylight Band Kila Ijumaaaa wewe uliekaa nyumbaniii njooo ufurahi nasiiiii Leo Ijumaaaaaa,ni mashabiki wa bendi wakiwa wanafurahia.